• Tukio 20 – Uchunguzi wa Wasikilizaji

  • Aug 25 2009
  • Durée: 15 min
  • Podcast

Tukio 20 – Uchunguzi wa Wasikilizaji

  • Résumé

  • Paula na Philipp wanawataka wasikilizaji kutoa maoni yao. Mada ya kipindi ni, "Je kusema uongo ni dhambi?" Wasikilizaji wanaweza kutoa maoni yao kuhusu maduara bandia ya mimea na tabia ya wakulima. "Je kusema uongo ni dhambi?" Paula na Philipp wanawauliza wasikilizaji. Swali hilo limetokana na matukio kwenye shamba la mahindi ambayo waandishi habari hao waliyatangaza. Je wakulima walaumiwe kwa vitendo vyao au watalii wanapaswa kujilaumu wenyewe kwa ujinga wao? Wasikilizaji wanaeleza mambo kinagaubaga. Tofauti na waandishi habari ambao wanauliza wasikilizaji maswali ya kujibu "ndiyo" au "la", mwalimu anatoa jukumu lenye uwezekano wa kushughulikiwa kwa jinsi tatu. Nomino za kijerumani zimo katika jinsia tatu: jinsia ya kiume, jinsia ya kike au bila jinsia. Haya yameelezwa katika tukio hilo pamoja na matumizi ya vidhihirisho "der," "die" na "das."
    Voir plus Voir moins

Ce que les auditeurs disent de Tukio 20 – Uchunguzi wa Wasikilizaji

Moyenne des évaluations de clients

Évaluations – Cliquez sur les onglets pour changer la source des évaluations.